Na Bazil Makungu
WENYEVITI wa Serikali za vijiji katika wilaya ya
Ludewa Mkoani Njombe wameitaka serikali kuwalipa posho au mishahara kwa kuwa
wanafanyakazi ngumu na katika mazingira ya hatari na yenye kila aina ya
ushawishi.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti
walisema kuwa wamekuwa wakifanyakazi ngumu zenye lawama na hatari na wakati
mwingine majira ya usiku kwa sababu tu ya kulinda usalama kwa wananchi.
Mzee Mwafute (56) ni mwenyekiti wa kijiji cha Lusitu
katika kata ya Madope Tarafa ya Mlangali kwa niaba ya wenyeviti wilayani
alisema wenyeviti wa vijiji pamoja na wenyeviti wa vitongoji ndiyo wenye watu
hata adha na usumbufu wanaopata hauna faida hata kidogo kwao na familia zao.
Kwa upande wake mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe
akaenda mbaili zaidi na kusema wanaotakiwa kulipwa posho siyo wenyeviti wa
vijiji na vitongoji tu bali hata wazee ambao wamelitumikia taifa hili lakini
hawakuwahi kuajiriwa wanatakiwa kutambuliwa kwa sababu wametoa mchango mkubwa
katika Taifa kwa namna moja au nyingine.
‘’’’ wenyeviti wa serikali za vijiji ni kweli kazi
wanazofanya ni ngumu kwa hiyo kinachotakiwa ni serikali kutambua uwepo wao na
kuonesha ukarimu kwa kuwapa posho kama siyo mshahara ili kutambua na kuthamini
kazi wanazofanya. Akashauri Filikunjombe
Akaongeza kuwa hata wakiwapa shilingi elfu tano ataona
tu umemtambua na siyo hao tu kuna wazee ambao wanalipwa pensheni baada ya
kustaafu serikalini lakini wapo wazee wale ambao walikuwa wakifanya kazi katika
sekta zisizo rasmi.
‘’’’ sisi tumekwenda zaidi ya hapo tumesema si hao
wenyeviti tu wanaostahili kulipwa, kuna wazee wanaopata pesheni kwa sababu
walikuwa watumishi wakastaafu, lakini tumesema hapana mtu yeyote ambaye saa
hizi ni mzee iwe alikuwa sekta isiyorasmi au rasmi maana yake ametumia nguvu
zake katika taifa hili akiwa kijana katika kuliendeleza taifa hili. Akafafanua
Mbunge huyo
Filikunjombe akaongeza kuwa idadi ya wazee
nchini inafikia milioni 4 tu nguvu zao zimetumika kwa hiyo kuna haja ya
kuainisha umri wa wazee hao wanaostahili kupata pesheni hata kama
ni shilingi ishirini elfu zinaweza kuwafariji.
Akatoa mfano kwa rais robert mgambe wa Zimbabwe ambaye
amejizolea sifa kwa kuwathamini na kutambua wazee lakini watu wake walikuwa
wanasoma bure kwa hiyo leo hii ukisema lolote juu yake wananchi wanatambua
jitihada zake.
Wenyeviti wa vijiji hawatakiwi kuacha kazi yao kwa sababu kazi hiyo
waliomba kwa kugombea kwa hiyo watakapofanya tofauti watakuwa hawajatenda haki
kwa serikali na kwa wale waliowachagua.
mwisho
No comments:
Post a Comment