Na Bazil Makungu
Ludewa
SHIRIKISHO la Vyama
vya wafanyakazi wa serikali (TUCTA)wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
wamewataka waajiri wa watumishi serikalini na wale wa mashirika ya umma
kutekeleza madai na stahili zao kwanza ndipo waweze kushiriki sherehe za mei
mosi mwaka huu.
Wakizungumza jana
katika mkutano wa shirikisho hilo viongozi na wawakilishi wa shirikisho hilo
wilayani Ludewa walisema wamechoshwa na unyanyasaji wanaofanyiwa na waajiri kwa
hiyo hakuna sababu ya kushiriki katika sherehe za mwaka huu kwani haina maana.
Joseph Mvanga ni
katibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi(TUCTA) wilaya ya Ludewa akifungua
mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa
alisema kila mwaka wamekuwa wakishiriki maadhimisho hayo na kuandika risara
ndefu lakini hakuna utekelezaji ‘’’’’ waajiri wamevaa miwani ya mbao na kuziba
masikio kwa pamba hawasikii kilio na madai yetu wala hawaoni taabu
tunazopata.’’’’’ Alilalamika Mvanga
Mvanga aliyataja
madai na kero wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja na watumishi kutopewa haki na
stahili zao wakati wa likizo,watumishi kukaa muda mrefu katika kituo kimoja,
kutopandishwa madaraja, kutolipwa malimbikizo baada ya kupandishwa madaraja.
Kero zingine ni
mahusiano mabaya kati ya wakuu wa idara na watumishi waliochini yao na ugumu wa
mawasiliano na wilaya, kutojibiwa barua kwa wakati na wakati mwingine
kutojibiwa kabisa hii ni kero inayokatisha tamaa.
Frolian Mvanginyi ni
mjumbe wa kamati tendaji ya chama cha walimu (CWT) tawi la wilaya ya Ludewa kwa
upande wake akaenda mbali zaidi na kusema wao wameomba kuonana na afisa elimu
tangu juni mwaka jana hadi leo hawajafanikiwa.
“”” maafisa na wakuu
wa idara wamekuwa wakikisema vibaya chama cha walimu utadhani wao siyo waalimu
na wamekuwa wakifanya uzembe wa makusudi wa kutowashughulikia walimu madai yao
ikiwemo maazimio ya vikao kutotekelezwa kwa wakati ili kufikia malengo.’’’’
Alilalamika Mvanginyi
Kuhusu watumishi
kukatwa michango mbalimbali kama mwenge kutoka katika mishahara bila ridhaa yao,
wajumbe viongozi wa tucta walikemea tabia hiyo na kusema huo ni udikteta na uuaji
kwa sababu hata taarifa ya mapato na matumizi ya makato hayo hayatolewi.
Naye mwalimu Samweli
Mputa aliitaka ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo
kuacha kuwapa watendaji majukumu mapya bila ya kutoa semina elekezi ili kuondoa
lawama linapotokea tatizo la utekelezaji hasa kuhusu fedha na uongozi.
‘’’’’’ sisi walimu wa
wilaya ya Ludewa idadi yetu inazidi 300 jambo la kushangaza afisa elimu wetu
ametenga siku moja tu ya ijumaa kama siku ya kushughulikia matatizo na
malalamiko ya walimu siku hiyo walimu hajaa katika ofisi hiyo bila mafanikio
hiyo ni kero kubwa kwetu tunaomba tuongezewe siku.’’’’’’ Akaongeza Mputta
Horace Kolimba ni
afisa utumishi katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa, akijibu baadhi ya
malalamiko na hoja za mkutano huo alikiri kuwepo kwa uzembe katika maeneo
kadhaa ikiwemo wakuu wa idara katika halmashauri yake kushindwa kuwafikishia
taarifa na maagizo yanayotolewa kutoka ngazi ya juu lakini akaahidi kufanya
mabadiliko na kutafuta mbinu mbadala za kuwasiliana na watumishi waliopo
vijijini kwa kutumia maafisa tarafa na maafisa watendaji wa kata.
Hata hivyo tucta
imemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuweka wazi fedha ya oc kwa kuzibandika
katika mbao za matangazo ili kuondoa kero na malalamiko. Hata hivyo viongozi
hao wametaka kuonana na mkuu wa wilaya hiyo ili kueleza kilio chao.
No comments:
Post a Comment