Kiongozi wa chama cha
wafanyakazi waserikali za mitaa Tanzania TALGWU amewaomba wanachama wa chama
hicho kupeleka taarifa za chama kila baada ya miezi mitatu
Akizungumzia suala hilo Beatrice Njawa ambaye ni katibu wa kamati ya wanawake
chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa taifa amesema ni jambo la msingi kwa
wanachama kushiriki katika vikao vinavyofanya ili kukusanya matatizo yao yaweze kushughulikiwa
Hata hivyo ameyataja
mafanikio ya chama hicho tokea kuanzia kwa mwaka 1995 chama kilikuwa na
wanachama elfu 4 na kufikisha wanachama elfu 75 hadi sasa katika mikoa yote ya Tanzania
Pamoja na mafanikio hayo Bi
Njawa amezitaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wa kazi
wa chama hicho kuwa ni baadhi ya wanachama kutoshiriki katika vikao vinavyokuwa
vimeandaliwa na viongozi wa chama katika ngazi ya wilaya hadi ngazi ya taifa
Katika hatua nyingine m/kiti
wa TALGWU wilaya ya makte Syprian Mahenge amewashukuru viongozi kutoka ngazi ya
taifa kwa kutoa elimu pamoja na ajira kwa wanachama wa chama hicho
No comments:
Post a Comment