Mwanafunzi aliyeshikwa akipandishwa kwenye Difenda. |
Utakwenda Tu! |
BAADA
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako
Kamanda
wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe
hoja zao
hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na
hayajashughulikiwa,
waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava
nakutaka
mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako
wanafunzi
wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa
maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada
ya hapo
ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa
walijeruhiwa
na kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata hivyo walioshikiliwa
wote waliachiwa
na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya
utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda
Kova
aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa
siku ya
tarehe 30 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment