Monday, January 14, 2013

MKUU WA WILAYA MAKETE AWAPIGA TAFU VIJANA


Mkuu wa wilaya ya makete mh Josophine Matro ameahidi kutoa kiasicha shilingi 160000 kwajili ya kuchangia mradi wa kilimo cha bustani na mazao mengine mradi huo ilibuniwa na wanamgambo wa Iwawa

 Akitoa ahadi hiyo Mh Matro mara baada yakuona jitiada za vijana hao walioanza kuchangia michango kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo unaotarajia kuanza kutekelezwa februar mwaka huu

Aidha Matro amewataka vijana wote wa makete kuacha utegemezi na badala yake wajiunge kwenye vikundi mbalimbali ili kujikwamua kiuchumu kupitia vikundi vya ujasiliamali kwani kufanya kutapunguza wimbi la vijana wengi kukaa kijiweni na maeneo mengine hatarishi

Hata hivyo vijana hao wamemshukuru nmkuu huyo wawilaya Makete kwa kuwapa hamasa na kuunganinisha  vijana hao toka walipo itimu mafunzo ya mgambo November mwaka jana na pia kwa kuanza kuwachangia ili kwani kufanya hivyo kunawajengea uwezo wqa kunza kufanya mladi huo na kuepukana  na utegemezi na kukua kiuchumi

Wilaya ya makete ni miongoni mwawilaya zinazo kabiliwa na vijana wengui kukosa ajira na kuwa tegemezi jambo ambalo linashusha maendeleo ya wilaya hiyo

No comments:

Post a Comment