SAKATA la maandamano yaliyofanywa na wananchi wa mikoa ya kusini kupinga mradi wa gesi, limekivuruga vibaya Chama cha Mapinduzi.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya serikali na chama hicho, zimesema kuwa umezuka msuguano mkali miongoni mwa viongozi wa serikali, kuhusiana na kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa hivi karibuni kupinga maoni ya wananchi wa mikoa hiyo kuhusiana na sakata hilo.
Wakati Rais Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na viongozi wengi wa CCM wakiwashutumu vikali wananchi walioandamana wakipinga kusafirishwa kwa gesi hiyo kwenda Dar es Salaam, taarifa zimebainisha kuwa mawaziri wengine wakisaidiwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, wamemgeuka mwenyekiti wao wakitaka maoni ya wana Mtwara yasikilizwe.
Chanzo chetu cha habari cha kuaminika ndani ya CCM, kimeiambia Tanzania Daima kwamba juzi mawaziri watatu (majina yanahifadhiwa), walikubaliana kwa dhati kulifikisha jambo hilo mbele ya vikao halali kufuta kauli ya Rais Kikwete na Profesa Muhongo, badala yake waangalie namna ya kutekeleza maoni ya wananchi hao.
“Kuna mvutano mkubwa mno. Hawa mawaziri wamekataa kabisa kukubaliana na hoja za Rais na waziri wake wa nishati na wanataka jambo hili litazamwe kwa uangalifu kwa sababu lina madhara makubwa kwa uhai wa serikali,” kimesema chanzo hicho.
Aidha chanzo hicho kimedai, mbali na mawaziri hao, wabunge wengi wa CCM tayari wametofautiana na kauli ya Kikwete na viongozi wengine wa CCM, wakisema kuwa hawakubaliana na mtindo wa serikali wa kupuuza mawazo ya wananchi, na kibaya zaidi wakisukuma lawama kwa viongozi wa vyama vya upinzani kwa madai yasiyokuwa na msingi.
“Unajua kama hatutaacha kusukuma lawama kwa wapinzani kwa kila jambo, bila kutambua kuwa hata wao ni Watanzania na wanayo haki ya kukataa jambo lolote wanaloona halina manufaa kwao, tutakuwa tunajichimbia kaburi na kupoteza heshima bure,” kilisisitiza chanzo hicho.
Hata hivyo, kuna habari kwamba tayari Rais Kikwete amefikishiwa ujumbe akiombwa kufuta kauli yake, na kukubali kukaa meza moja na wazee wa mikoa ya Mtwara na Lindi kujadiliana namna njema ya kutekeleza mradi huo kwa manufaa ya Watanzania wote.
“Mzee wamempelekea taarifa mbaya na zisizo na ukweli. Hawa Watanzania wenzetu, hawajakataa mradi huu, bali wanachosema wao, mtambo ujengwe Mtwara kwenyewe, na umeme usambazwe kutoka hapo, ili nao wanufaike na mradi huo wa umeme badala ya gesi hiyo kusafirishwa hadi Dar es Salaam,” kilifafanua zaidi chanzo hicho.
Wakati msuguano huo ukiendelea, wiki hii Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Mohamed Sinan amesema wanapongeza msimamo wa Kikwete alioutoa wakati wa kutoa hotuba ya mwisho wa mwaka, wa kujenga bomba la kusafirisha gesi asilia toka Mtwara hadi Dar es Salaam.”
Msimamo huo wa Rais Kikwete, ulirudiwa kwa namna isiyovutia na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Waziri Muhongo, aliwakejeli wakazi wa mikoa hiyo akisema hawakuwa na sababu ya kuandamana kutaka gesi asilia iwanufaishe kwa kuwa mikoa hiyo haina uchumi utakaoweza kutumia gesi hiyo.
Prof. Muhongo pia aliwakejeli wanasiasa waliounga mkono maandamano ya wakazi hao, akiwemo mbunge wao wa Mtwara Mjini, akisema kuwa wanapaswa wajue kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara haina gesi inayomiliki.
“Hiyo gesi inayowafanya wanasiasa wawashawishi wakazi wa Mtwara kuandamana haiko Mtwara wala Lindi, bali iko katika mipaka ya Tanzania ndani ya kina kirefu cha bahari na kwa hilo kila Mtanzania ana haki ya kutumia,” alisema na kuwashambulia wabunge wa maeneo hayo, akisema kuwa walikuwa wamepelekwa semina nje ya nchi kwa ajili ya masuala ya gesi na wamelipwa posho hivyo aliwashangaa kwa msimamo huo.
Wananchi wa Mtwara waliandamana Desemba 27, 2012, kupinga kusafirishwa kwa gesi asilia kupelekwa Dar es Salaam, msimamo ambao pia uliungwa mkono na Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia chama hicho Husnain Murji.
Akijibu kuhusu msimamo wa Prof. Muhongo alisema: “Kwanza namshukuru waziri kwa kunipeleka kujifunza Trinidad na Tobago, nilichojifunza ni kwamba wenzetu wa huko wana uzoefu wa miaka 100, na wanawajali watu wa eneo husika ambako rasilimali inatoka tofauti na sisi tunavyotaka kuwafanyia wakazi wa Mtwara,” alisema.
Aliongeza kuwa wananchi wa Mtwara ni lazima wajue watanufaika vipi na rasilimali ya gesi kwa kile alichoeleza kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, alipofika mkoani humo katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, aliwaambia hawana chao katika mrahaba mzima wa gesi.
Murji aliongeza kuwa kazi ya mbunge ni kusikiliza mawazo ya wananchi na alichoeleza ndio msimamo wa wananchi, huku akisisitiza kuwa Waziri Muhongo amedanganya kwani wakazi wa Mtwara hawajawahi kunufaika na umeme wa kutoka nje ya Mtwara.
Alihoji ulazima wa serikali kujenga mtambo wa gesi Kinyerezi jijini Dar es Salaam na kuacha kuzalisha umeme huo mjini Mtwara na kisha uunganishwe katika gridi ya taifa.
Hivi karibuni, Waziri Mkuu mstaafu na mwanasiasa mkongwe nchini, John Malecela, aliishauri serikali ifanye kila iwezalo ili wakazi wa Mtwara wananufaika kwanza na rasilimali hiyo.
“Ukiwa karibu na waridi unatakiwa kunukia waridi. Wakazi wa Mtwara nao wanatakiwa wanukie waridi,” alisema Malecela na kuongeza kuwa ukweli wakazi wa eneo inakopatikana rasiliamali hiyo wanapaswa kunufaika nayo, haukwepeki.
“Hatutakiwi kuwaacha hivi hivi wana Mtwara eti kwa sababu hii ni rasilimali ya Watanzania wote. Serikali iyaangalie kwa umakini maeneo yanayotoa utajiri na rasilimali, ni lazima wapewe upendeleo ili wafurahie matunda ya mali asili yao.
Msimamo huo ulifanana pia na wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ambaye alililalamikia serikali kuwa inasisitiza kujenga mitambo Kinyerezi kwa kuwa wanataka kuleta gesi hiyo Dar es Salaam ili kunufaika wao kwanza, jambo ambalo ni la kiubaguzi.
“Wananchi wa Mtwara ni maskini, mkoa wao umetelekezwa muda mrefu, wamekopwa korosho yao, sasa wamepata gesi na wanayo haki ya kudai wanufaike nayo ili nao wapate viwanda, shule na hospitali nzuri.
Dk. Slaa alisema mikoa hiyo haijawahi kuwa na hospitali ya rufaa, hivyo wanaionya serikali isiendeshe shughuli za uchumi kwa maslahi ya watu wachache.
Alisisitiza kuwa hakuna sababu ya kutokuwekeza mitambo ya gesi Mtwara na Lindi ili isaidie ukuaji wa maeneo hayo kiuchumi na kwamba jambo hilo wala halina siasa.

No comments:
Post a Comment