MTI WAANGUKA MLIMA IPOGOLO MAGARI YAKWAMA KUPITA
Wananchi wakisubiri mti kutolewa barabarani baada ya kuanguka na kuziba barabara ya mlima wa Ipogolo mjini Iringa leo jioni
Hapa wananchi wakihangaika kukata mti huo kwa shoka ili kupata nafasi ya kupita
Msamaria mmoja akikata mti kwa shoka huku mwendesha pikipiki akijaribu kupenya eneo hilo
Foleni ya magari ikiwa imekwama eneo hilo leo
Mzungu ambae ni mfugaji Bw Philip akiwa amejitolea mashine ya kukata mti huo na hapa kazi ikianza
Hapa akiwa ametoa mashine ya pili kukata mti huo
Wananchi wakishindwa kupita eneo hilo
Kazi inakwenda
Abiria wakiwa wamekwama eneo hilo
Askari polisi wakiweka ulinzi eneo hilo
Baadhi ya abiria wanapoamua kutembea kwa miguu
Hapa zoezi la kuvuta magogo yaliyokatwa na mzungu mwema huyu
Hivi ndivyo mti ulivyong'oka
Zoezi likifikia ukingoni
Tukio hilo limetokea mida ya saa 8 mchana katika eneo hilo ambapo moja kati ya daladala lililokuwa likipandisha eneo hilo likiwa na abiria zaidi ya 50 limenusurika kufunikwa na mti huo.
Baadhi ya abiria na mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com eneo la tukio wamedai kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa japo wameomba wasimamizi wa barabara hiyo wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADS) kuangalia uwezekano wa kukata miti mikubwa iliyopo eneo hilo ili kuepusha maafa makubwa zaidi ya hayo.
Kwani wamesema tatizo la mti huo na mawe kuanza kuporomoka katika mlima huo limetokana na baruti ambazo zilikuwa zikitumika kupasua mawe katika mlima huo wakati wa upanuzi wa barabara hiyo hivyo sasa maji yanapoingia ndani ya ardhi hiyo ndio husababisha matatizo hayo .
Baadhi ya wananchi wamempongeza meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa Paul Lwakurwa kwa kufika mapema eneo hilo na kufanikisha kutatua tatizo hilo vinginevyo hadi kesho barabara hiyo ingefungwa rasmi.
No comments:
Post a Comment