MATUKIO YA UPANDAJI MITI WILAYANI MAKETE KATIKA PICHA
Baadhi ya miti iliyopandwa siku ya leo
Mgeni rasmi akipanda mti wake
Afisa maliasili na mazingira wilaya ya Makete Uhuru Mwembe akipanda mti
Mwakilishi wa CHADEMA Makete akipanda mti
Mfuasi mwingine wa CHADEMA naye alipanda mti
Mwakitalima kutoka shirika la SUMASESU akipanda mti wake
Mkurugenzi wa SUMASESU na Diwani wa kata ya Tandala Egnatio Mtawa akipanda mti
Mwanahabari kutoka kitulo fm na mmliki wa blog ya eddy mo blaze hakuwa nyuma kupanda mti
Wananchi wakiwa wametawanyika kupanda miti kwenye eneo hilo
Wanafunzi nao hawakuwa nyuma
Chanzo cha Maji cha Ng'wenyo ambapo pamepandwa miti hii leo
Maji yameonekana kupungua kwenye chanzo hicho
Jumla ya miti 4377 imepandwa katika eneo la Tandala wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kiwilaya ambayo yalifanyika katika kata ya Tandala.
Upandaji huo ulizinduliwa na katibu tawala wa wilaya bwana
Onesforia Ngogo kwaniaba ya mkuu wa wilaya ya Makete na baadaye kuendelea
kupanda miti hiyo ilyofikia idadi yake 4377 ambapo halimashauri ilitoa jumla ya
miti 2665 huku diwani wa Tandala mh Egnato Mtawa akitoa miti 1119 na udiakonia walitoa miti
521
Baada ya uzunduzi huo bwana Ngogo alisoma hotuba ya mkuu wa wilaya Makete MH Josophine
Matiro ambapo amesema kila ifikapo tarehe kumi ya mwenzi wa kwanza wilaya ya
Makete huadhimisha siku ya upandaji miti kiwilaya na kama
wilaya imeweka lengo la kupanda miti 9,000,000 kila mwaka
Aidha MH Matro amesema kuwa serikali imekuwa ikitoa elimu
pamoja na uhamasishaji wa upandaji miti kila mwaka ambapo mwaka 2012wilaya
ilikuwa na lengo kupanda miti milioni sita ambapo ilifanikiwa kupanda miti
milioni saba na laki nne hamsini na sita elfu
na kuongeza kuwa wananchi waendelee kuunga mkono juhudi hizo kwakuto
choma moto nyakati za kiangazi
Katika hatua nyingine
MH Matro aliwaasa wananchi kutopanda miti hadi kwenye mashamba ya mazao
kwani kufanya hivyo kuna hatarisha maisha ya wanamakete kwani wanaweza kukumbwa
na njaa kutoka na uhaba wa mashamba ambayo watu wamekuwa wakipanda miti bila
kutenga maeneo ya kilimo vilevile kuacha
kuvuna miti michanga ambapo inapelekea wanachi kutopata faida stahiki
Kaulimbiu ya mwaka huu panda miti kuitunza ongeza kipato cha
kaya na hifadhi ya mazingira
No comments:
Post a Comment