Simba SC |
MABINGWA wa
Bara, Simba SC wanatarajiwa kuondoka leo Dar es Salaam kwenda Oman kuweka kambi ya
wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kuhusu Kombe
la Mapinduzi, Simba imegawa vikosi viwili na kile ambacho kilichukua Kombe la
Sup8R Banc ABC kwa kuzifunga Azam FC na Mtibwa Sugar ndicho kitabaki kwenye
Kombe la Mapinduzi chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Mganda Richard
Hamatre.
Kikosi hicho
cha Mapinduzi kina wakali kama Ramadhan Singano ‘Messi’, Edward Christopher,
Abdallah Seseme, Haruna Chanongo, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Miraj Adam na
wengine ambao wote wanachezea Simba A.
Wachezaji wanaobaki
kwenye Kombe la Mapinduzi, watakwenda Oman baada ya mashindano hayo pamoja na
kocha Julio.
Simba SC
kesho inatarajiwa kumenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi
kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mchezo huo
utakuwa ni marudio ya Nusu Fainali ya mwaka jana, ambayo Azam FC waliitoa Simba
SC kwa kuichapa mabao 2-1.
Kocha Msaidizi
wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali,
amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali kuliko
Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.
Ikiwa Oman,
Simba itakaa kwa wiki mbili na itacheza mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya
timu ambazo wameandaliwa na wenyeji wao Fanja FC. Aidha, wameandaliwa makocha
watatu huko, wakiongozwa na beki wa zamani wa Simba SC, Talib Hilal kuungana na
makocha wa Simba kuinoa klabu hiyo ikiwa nchini humo.
Hiyo ni ziara
ya mafunzo, ambayo lengo lake ni kuiweka sawa Simba SC kabla ya kuanza kwa
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
No comments:
Post a Comment