Mtoto anayesomeshwa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Geita, Josephine Chagula ameachishwa masomo na kuozeshwa.
Taarifa hiyo iliyomuumiza mbunge huyo, ilitolewa
jana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi katika Wilaya ya Mbogwe, Julius
Masubwa.
Masubwa ambaye pia ni Mbuge wa Bukombe alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumzia watoto wanaosomeshwa na mbunge huyo.
Alisema msichana huyo aliyekuwa miongoni mwa
watoto kumi waliokuwa wakigharimiwa na mbunge huyo katika masomo yao,
ameozeshwa na wazazi wake Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, msichana huyo
alikuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Lubungo.
Alisema kwa kipindi kirefu alikuwa haudhurii
masoma jambo lililoulazimisha uongozi kufuatialia na hatimaye kubaini
kuwa ameozeshwa.
Ofisa Elimu ya Sekondari wilayani humo, Philbert
Nyangahondi alisema alipata taarifa hizo lakini hana uhakiki. Alisema
hata hivyo atalifuatilia na kwamba tatizo la utoro katika wilaya hiyo
ni kubwa na kwamba linachangia na wazazi kutoona umuhimu wa kusomesha
watoto.
Akikabidhi vifaa vya shule kwa ofisa elimu huyo
Chagula alisema kitendo alichokifanya mzazi huyu ni cha kinyama na
kuagiza mamlaka husika kuhakikisha kuwa mwanafunzi huyo anarudi shule
..mara moja na aliyemuoa, hatua za kisheria zichukuliwe.
“Natumia gharama zangu kuwasaidia watoto wa kike
wanaoishi kwenye mazingira magumu lakini watu wanawaachisha shule,
nimeumia sana ofisa naomba suala hili lishughulikiwe haraka sana,”
alisema Chagula.
Chagula anasomesha watoto 30 katika Mkoa wa Geita na katika Wilaya ya Mbongwe anasomesha watoto 10.
No comments:
Post a Comment