Sunday, January 13, 2013

ASAMOAH GYAN AKATARIWA KUPIGA PENATI





NAHODHA wa Ghana, Asamoah Gyan amesema hatopiga penalti katika muda wa kawaida wa mchezo wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika zitakazoanza kutimua vumbi nchini Afrika Kusini wiki ijayo.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27, alikosa penalti iliyowanyima Ghana nafasi ya kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Dunia 2010 na akakosa tena kwenye nusu fainali ya Kombe la Afrika mwaka jana.
Baada ya kitendo hicho mshambuliaji huyo alijikuta kwenye wakati mgumu kutoka kwa mashabiki na kusababisha ajiuzulu kuichezea timu ya taifa kwa muda, lakini sasa Gyan ameamua kutopiga kabisa penalti.
“Nimeamua kutokuwa mpigaji wa penalti wa timu ya taifa,” alisema.
“Wachezaji wengi mashuhuri wanakosa penalti kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Diego Maradona. Ikiwa siku yako mbaya utakosa.
“Lakini nilishasema mwezi moja uliopita kuwa sitopiga tena penalti. Kabla ya mama yangu hajafariki mwezi Novemba aliniambia nisipige tena penalti.”
Miaka miwili iliyopita Gyan alishindwa kufunga penalti dhidi ya Uruguay kwenye dakika za mwisho za mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia, na kama wangeshinda mchezo huo basi Ghana ingekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa nusu fainali kwenye historia ya mashindano hayo.
Pia, Februari 2012, Gyan alikosa penalti iliyoinyima nchi yake kufuzu kwa nusu fainali d
hidi ya

No comments:

Post a Comment