Timu ya Young Africans Sports Club
iliyokuwa imeweka kambi ya wiki mbili katika mji wa Antalay nchini
Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya
vodacom na mashindano ya kimataifa tayari imeshatua nchini leo aflajiri.
Msafara wa watu 33 ukiwa na wachezaji 27
na viongozi 6 umewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa majira ya
saa 10 kasoro alfajiri kwa shirika la ndege la Uturuki Turkish Air
ambapo katika mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako aliongoza
mapokezi hayo.
Young Africans iliweka kambi katika
hoteli ya Fame Residence kwa kipindi chote cha mafunzo ambapo pia
ilipata fursa ya kucheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu na timu kutoka
barani ulaya katika nchi za Uholanzi, Uturuki na Ujerumani.
Mara baada ya kutoka nje ya uwanja wa
ndege bus la klabu liliwachukua wachezaji na viongozi tayari kwa kwenda
kupumzika ambapo kocha mkuu Ernest Brandts ametoa mapumziko ya siku 2
kwa wachezaji kukaa na familia zao kabla ya kuanza mazoezi tena siku ya
jumatano kujiandaa na ligi ku ya vodacom.
No comments:
Post a Comment