Sunday, January 13, 2013

ANGALIA PICHA ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAPINDUZI WILAYANI MAKETE






 Wakati mkuutano ukiendelea huyu nae kala pozi lake
Mmiliki wa mtandao wa eddymoblaze blogspot akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati wageni wakiwasili kwenye viwanja vya Nungu





Viongozi wa kata na vijiji wilayani Makete wameagizwa kuwasomea wananchi wa maeneo yao mapato na matumizi ya fedha wanazozichanga kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kuondoa minung’uniko waliyo nayo wananchi na imani potofu kuwa fedha zao zimechakachuliwa

Endapo hali hiyo itafanywa pia itasaidia wananchi kuzidi kuwa na moyo wa upendo wa kuchangia miradi mbalimbali pamoja na kuwa na imani na serikali yao

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete mh Danieli Okoka ya maadhimisho ya miaka 49 ya mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji cha Nungu kata ya Matamba wilayani hapo

Amesema wakati hayati rais Amani Karume anafanya mapinduzi huko Zanzibar kuondoa utawala wa kisultani, shughuli mbalimbali za kimaendeleo zilifanyika ikiwemo ujenzi wa taasisi mbalimbali hali iliyofanywa kwa uwazi na kuwashirikisha wananchi kwa uwazi

“kule Zanzibar kuna majengo makubwa tuu yaliyojengwa tangu miaka ya 1970 na ukiyatazama hadi leo utafikiria yamejengwa jana, hakukuwa na uchakachuaji na ndio maana unaona hadi leo yapo imara, na ndio maana na nyie watendaji mnatakiwa kuwaweka wazi wananchi wenu kwa kila fedha wanayoitoa imetumikaje” alisema

Katika hotuba yake hiyo pamoja na mambo mengine iligusa sekta mbalimbali zikiwemo elimu, utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa na Ukimwi huku kila nyanja ikielezewa changamoto na mafanikio

Maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar huadhimishwa Januari 12 ya kila mwaka kwa lengo la kukumbuka juhudi za aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amani Abeid Karume za kuondoa utawala wa kisultani visiwani humo

No comments:

Post a Comment