Friday, January 11, 2013

KIONGOZI WA MAHARAMIA SOMALIA ASTAAFU


Kiongozi mmoja wa kijamii nchini Somalia, ameiambia BBC kuwa, mtu mmoja ambaye ametanjwa na Umoja wa Mataifa, kuwa kinara wa utekaji nyara, ametangaza kuwa amestaafu rasmi kutoka kwa uharamia.

Mohamed Abdi Hassan, ambaye anajulikana kwa jina la utani kama "afweyneh" ikiwa na maan mtu mwenye usemi mkubwa nchini Somalia, amewaambia waandishi wa habari kuwa anastafu kutoka kwa biashara hiyo baada ya miaka minane.
Bwana Hassan aliyasema hayo katika kikao kilichofanyika mjini Abado, kati kati mwa Somalia, eneo ambalo maharamia hao wamekuwa wakiwazuilia mateka wao

No comments:

Post a Comment