Thursday, January 17, 2013

ALIYE JIFANYA HAKIMU WA WILAYA MIKONONI MWA BCCB

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mbeya imewakamata na kuwafikisha mahakama ya Wilaya ya Rungwe, hakimu wa mahakama ya mwanzo ya Kata ya Lupata Andrew Siwale na afisa mtendaji wa kata ya Kisegese Gasper Bagomoke kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa pamoja na vitendo vya uonevu hasa kwa watu wasio na kipato.

Wananchi wa eneo husika wamesema watendaji wa kata hiyo wamekuwa wakimtoza faini mwananchi hadi shilingi laki tatu kwa kosa moja na kuteswa kwa mwananchi asiyekuwa na kipato cha kutosha cha kulipia faini.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata hiyo Bwana Bagomoke amekiri kuwa hakimu huyo kuchukuwa fedha kwa watuhumiwa wanaobainika na makosa mbalimbali na kuwaagiza Migambo kuwanyanyasa wananchi pamoja kuwatoza faini kwa kuwapandikizia kesi.

Aidha, akiongelea sakata hilo Mkuu wa Taasisi ya hiyo mkoani hapa Daniel Mtuka amesema viongozi hao wamekamatwa January 15 katika maeneo mawili tofauti mmoja akiwa Kata ya Kisegese na mwingine kata ya Itete na kasha kuhojiana nao na kupata ushahidi.
CHANZO: BOMBA FM

No comments:

Post a Comment