Ilikuwa ni Sinza mama huyu alitupwa
nje ya nyumba baada ya kuvamiwa na mabaunsa chini ya usimamizi wa
polisi.Ambapo mama huyu alisema mtu aliyenyuma ya tukio hilo ni
aliyekuwa mume wake.
Tukafatilia kwa kumpigia kamanda wa
polisi kanda ya Kinondoni na mkuu wa kituo cha polisi osterbay ambako
polisi walitoka huko kusimamia zoezi la kuhamishwa mama huyu.Tukaambiwa
wao walipata barua kutoka mahakamani kuwa wanahitajika kusimamia ulinzi
wakati mpangaji wa nyumba hiyo akitolewa nje.Mwanasheria wa huyo mama
anasema wana kesi mahakamani kati yake na huyo mume ambayo haijaisha na
inatarajiwa kusikilizwa kwa mara ingine tarehe 2 mwezi ujao.Na mbaya
zaidi yeye hajapewa taarifa kuwa ahame ila amevamiwa.
Vitu mbali mbali vikiwa nje baada ya kutolewa nje na ndani kuwekwa mabaunsa kulinda asiingie mtu.
Kama kuna kitu kiliniuma ni huyu bibi
pichani.Huyu ni mama wa huyo dada na bibi wa watoto hao ambao walikuwa
likizo muda wote shule zilipofunga.Bibi ndio alikuwa amewaleta
wajukuu zake na kuishia kushuhudia mwanae akitupwa nje na mabaunsa
akiwemo na yeye ni udhalilishaji wa hali ya juu.Nilikuwa namuangalia
bibi wa watu na machozi kunilenga majirani wanasema hata kula hakuwa
akitaka kula amekaaa kimyaa tu.
Jioni majirani wakamsaidia kuhifadhi vitu kwenye nyumba zao
Mwenye kubeba kabati,vifurushi vya nguo,vyombo ilimradi wamsitiri mwanamke mwenzao.
Usiku majirani walifanya fujo sana
kiasi cha mapolisi kuingilia kati...ishu ilikuwa huyo anaedai ndio
mwenye nyumba ajitokeze.Alikuja mpaka diwani wa eneo hilo polisi pia
wakaja kuwatoa hao mabaunsa na mama wa watu kurudishwa ndani ya nyumba.
Jana aliamkia mahakamani na mahakama
kuamua akae kwenye hiyo nyumba bila kubugudhiwa mpaka kesi yao
itakapoisha.Sikiliza heka heka ya leo utakisikia kisa hiki.
No comments:
Post a Comment