Thursday, January 17, 2013

AFCON LIVE KUPITIA DStv !




Michuano ya kuwania Ubingwa wa Afrika kwa upande wa soka; Orange Africa Cup Of Nations, inaanza kurindima kutokea nchini Afrika Kusini Jumamosi hii(tarehe 19 Januari). Jumla ya timu za taifa kutoka mataifa  16 zinatarajiwa kuteremka dimbani ili kupata mbabe katika mchezo wa soka ambao ndio maarufu kushinda michezo yote barani Afrika.

Kuanzia kipyenga cha kwanza kitakapopulizwa kutoka katika Uwanja wa Taifa(National Stadium) wa jijini Johanesburg mpaka kipyenga cha mwisho tarehe 10 Februari katika uwanja huo huo, mashabiki wa soka barani Afrika na kote kwingineko watashuhudia jumla ya mechi 32.

Mshindi wa michuano hii licha ya kupata heshima ya kuwa mbabe wa soka barani Afrika, atakuwa pia amekata tiketi ya kuliwakilisha Bara la Afrika katika Michuano ya kuwania Ubingwa wa Dunia(World Cup) hapo mwakani nchini Brazil katika kundi B ambalo tayari lina timu za Spain, Uruguay na Tahiti.

Iwe ungependelea kutizama mechi zote ukiwa nyumbani kwako au ukiwa mtaani sehemu ya kujumuika na wenzako, DStv kupitia channels zao za michezo za Super Sports ndio pekee ambao wanaweza kukupa uhakika wa kushuhudia mechi zote Live.

Nasi kwa kushirikiana na DStv, tutakuwa katika sehemu(mikoa) mbalimbali nchini Tanzania ili kutizama fainali hizi pamoja nawe mshabiki na mpenzi wa soka. Tutapenda kuzungumza nawe, kucheka nawe na hata ikibidi kulia pamoja(Ndio, upenzi wa soka waweza kumliza mtu hususani pale mambo yanapokwenda Ndivyo Sivyo )

Nchi na timu ambazo zimefanikiwa kuingia katika fainali hizo ni Afrika Kusini, Ghana, Mali, Zambia, Nigeria, Tunisia, Ivory Coast, Morocco, Ethiopia, Cape Verde, Angola, Niger, Togo, Congo DR, Burkina Faso na Algeria

Timu hizo zimegawanywa katika makundi manne(4) kama ifuatavyo;

Kundi A

Afrika Kusini
Angola
Morocco
Cape Verde

Kundi B

Ghana
Mali
Niger
Congo DR

Kundi C

Zambia (Mabingwa Watetezi)
Nigeria
Burkina Faso
Ethiopia

Kundi D

Ivory Coast
Tunisia
Algeria
Togo

Soccer City(National Stadium, Johannesburg, Uwanja ambapo ndipo mechi ya Ufunguzi na ile ya Fainali zitafanyikia.
Je, unaunga mkono au ungependelea timu gani inyakue Kombe mwaka huu? Na je,unadhani Zambia(The Chipolopolo) wataweza tena kufanya kile walichokifanya mwaka jana walipofika fainali za michuano hiyo na kuwatandika Ivory Coast iliyokuwa imesheheni mastaa kama Didier Drogba nk? Endelea kufuatilia kurasa hizi za BC na pia jiunge leo na Ukurasa maalumu Facebook wa DStvTanzania kwa kubonyeza hapa. Let the games begin!

No comments:

Post a Comment