Mkurugenzi
wa habari nchini Habi Gunze amesema Vituo vya Redio ambavyo ni
chochezi, vitachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kuvifugia.
Gunze
ametoa kauli hiyo juzi, mada mfupi uliopita mara baada yakupokea taarifa
fupi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, kufuatia
Kamatia ya Bunge iliyozuru Mkoani humo .
Gunze
amesema vituo ambavyo huenda vikafungiwa ni pamoja na vile vinavyo
eneza na kufanya uchochezi wa waumini wao kwakutumia mwamvuli wa dini.
Awali akitoa taarifa Mbele
ya kamati ya Bunge inayoshughullikia huduma za jamii Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza amesema katika siku za hivi karibuni kituo cha Kwa Neema Fm cha
jijini Mwanza na kile cha Redio Imani kilichopo Mkoani Morogoro vimekuwa
vikienda kinyume na utaratibu na hivyo kuweka rehani Amani ya Nchi.
Akizungumzia
kuhusu Kwa Neema Fm amesema, kituo hicho kimekuwa kikirusha matangazo
yake nakuwashawishi Wakristo kuchinja nyama, badala yakuwapelekea wenzao
waislamu.
Kwa
upande mwingine Ndikilo amesema, kituo cha Redio Imani kilitumika
vibaya wakati azoezi la Sensa ya watu na maakazi ilyofanyika nchini kote
Agosti 26 mwaka jana wa 2012.
Kamati ya Bunge kuhusu huduma
za jamii ipo Mkoani Mwanza kwa Ziara ambapo pamoja na mambo mengine
itatembelea chuo cha Michezo Malya, Vituo vya Redio Free Afrika na Star
TV pamoja naTBC Mwanza.
NA
ATLEY KUNI- AFISA HABARI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
No comments:
Post a Comment