Vituo vinavyolelea watoto yatima wilayani Makete
vimetakiwa kubuni na kuanzisha miradi endelevu itakayosaidia vituo hivyo kuzidi
kutoa huduma bila kutegemea wahisani mbalimbali
Imeonekana kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia vituo hivyo
kuendelea kuwepo hata kama wafadhili hao
watasitisha ufadhili katika vituo hivyo, miradi waliyobuni na kuitekeleza
itasaidia kuendesha vituo hivyo
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete Mh.
Josephine Matiro wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Fema Matamba
kwa lengo la kutoa msaada kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho
Alisema huu sio muda wa kubweteka na kuwategemea wafadhili
pekee badala yake ni kuangalia mbele zaidi kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama kilimo ambvyo itasaidia kuleta kipato cha vituo
hivyo hasa ukizingatia hivi sasa wahisani wengi wanaanza kujitoa kufadhili
masuala mbalimbali
Hata hivyo mkuu huyo amepongeza uongozi wa kituo hicho kwa
kuwa na moyo wa kusaidia kulea watoto hao yatima ambao mara nyingi jamii imewasahau,
na kusema kuwa malipo ya kazi yao
yatatolewa na mwenyezi MUNGU
Awali akitoa maelezo kuhusu kituo kwa Mh. Mkuuwa wilaya,
msimamizi wa kituo hicho cha Fema Matamba Bi.Ala Mbwilo alisema kituo hicho
kinategemea msaada wa wafadhili waliopo nje ya nchi ambao hutoa sh. Milioni 2
kila mwaka fedha ambazo bado hazitoshi kuendesha kituo hicho
Pamoja na hayo alisema ukosefua wa maji nalo ni tatizo
lililopo eneo la Matamba ambalo huwalazimu kwenda mtoni kuchota maji ama kwenye
bomba za vijiji jirani kwa ajili ya mahitaji ya kituo hicho
Naye Askofu wa dayosisi ya kusini magharibi ambayo
inamiliki kituo hicho Job Mbwilo ameshukuru kwa ujio huo wa mkuu wa wilaya huku
alisema yeye ni kiongozi wa kwanza kufanya ziara ya kutembelea kituo hicho na
kutoa msaada kwa watoto yatima wanaoishi hapo
Alisema wazo alilolitoa la kituo hicho kuwa na miradi
endelevu watalifanyia kazi haraka iwezekanavyo kama
namna ya kuboresha kituo hicho kwa kuwa jukumu la kuhakikisha watoto yatima
popote duniani ni la jamii nzima, hivyo jamii nayo inapaswa kushirikiana kwa
pomoja kuwalea watoto hao
Mh Matiro alitoa kilo 50 za
sukali,unga wa ngano kilo 25,mafuta ya kupikia lita 10,unga wa sembe kilo
25,sabuni ya kufulia katoni 1,dawa za meno katoni 1 na soda kreti 1.
No comments:
Post a Comment