Friday, December 14, 2012

NAIBU WAZIRI WA MAJI DKT MAHENGE AFANYA ZIARA JIMBONI MWAKE



Wakazi wa kata ya Kipagalo wilayani Makete wametakiwa kutunza barabara zilizopo katani humo ili ziweze kuwaongezea kipato
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa maji na mbunge wa jimbo la Makete Mh. Dkt Binilith Mahenge na kuongeza kuwa serikali bado inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi mzuri wa barabara katani humo
Amesema njia inayotumika kwa ajili ya shughuli za utalii kutoka Kipagalo hadi Matema ikitengenezwa na kukarabatiwa vizuri itaongeza kipato kwa wananchi wa kata ya Kipagalo na halmashauri kwa ujumla
Mh Mahenge amesema mbali na barabara pia serikali inampango wa kuweka umeme wa gridi ya taifa katika vijiji 22 vya wilaya ya Makete hivyo wananchi wavute subira na muda si mrefu wataondokana na kero ya kukaa kwenye giza
Katika ziara hiyo mheshimiwa naibu waziri amkabidhi vitabu vya masomo mbalimbali ikiwemo hesabu, kiingereza na sayansi kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Kipagalo
Naye afisa elimu sekondari wilaya ya makete Bw. Jacob Meena ameshukuru kwa msaada huo uliotolewa na Naibu waziri kwa shule yake na kuwataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana na waalimu kwa lengo la kuinua taaluma shuleni hapo, huku akisema bado wilaya inachangamoto ya waalimu wa masomo ya sayansi
Ziara ya naibu waziri katika jimbo lake inaendelea katika kata ya Iwawa kwa kutembelea vijiji vya Ivalalila, Ndulamo na Iwawa

No comments:

Post a Comment