Sunday, December 30, 2012

VIDEO YA DIAMONDI KESHO KITAA

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Kesho’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Tanzania Daima Dar es Salaam jana, Diamond alisema kazi hiyo ameshaisambaza katika vituo mbalimbali vya runinga ambapo ana uhakika vimeshaanza kuufanyia kazi wimbo huo.
Alisema anawaomba mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake ili aendelee kuwapa burudani ya hali ya juu wapenzi na mashabiki wake.
“Kama mnavyojua mimi ndiye mkali wa Tanzania, hivyo hata vitu vyangu lazima viwe vikali, kazi hii nimeifanya vizuri na mtayarishaji Adamu Juma ambaye huwa hafanyi utani katika kazi zinazopitia kwake,” alisema Diamond.
Alisema kawaida yake anaachia wimbo baada ya kutoa wimbo hivyo kwasasa yupo katika matayarisho ya kuachia kibao kingine hivyo mashabiki wake mkao wa kula.
Kwa sasa Diamond anatamba na kibao chake kinachokwenda kwa jina la ‘Nataka Kulewa’ kinachofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na luninga.

No comments:

Post a Comment