Sunday, December 30, 2012

BEN POL KUFUNIKA CLUB BILICANAS LEO



MSANII wa muziki wa bongo fleva, Ben Pol, leo anatarajiwa kutoa burudani ya nguvu katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mmoja ya viongozi wa ukumbi huo, Hamis Omary, alisema usiku huo utakuwa wa aina yake kutokana na kusindikizwa na matukio tofauti katika kukamilisha burudani hiyo ya nguvu.
Alisema, burudani hiyo ya Ben Pol itakayofanyika kupitia usiku wa ‘Bongo Starz’ unaorindima kila Jumapili na kupambwa na wasanii nyota itakuwa ya kufunga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013.
“Kutokana na kuwajali na kuwathamini mashabiki wetu ndiyo maana tumeamua kuwaletea Ben Pol ili aweze kukidhi haja zao, nawaomba wajitokeze kwa wingi katika onesho hilo kwa kiingilio cha sh 6,000 tu,” alisema.
Ben Pol ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya mwanamuziki bora wa R&B ambapo kwa sasa anatamba na singo ya Pete, amewahi pia kuachia singo zilizoweza kushika chati za juu katika bongo fleva zikikiwamo, Nikikupata, Samboira, My Number One Fun, Yatakwisha na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment