Imeelezwa kuwa tatizo la umasikini hapa nchini kwa kiasi
kikubwa linachangiwa na wananchi wengi kutegemea kipato sehemu moja
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa vijana taifa Dkt. Kisui
Steven wakati akifundisha masomo ya ujasiria mali kwa baadhi ya wananchi wa
makete waliohudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya
sekondari Iwawa
Amesema wananchi wengi hasa vijana wamekuwa wakibweteka na
kutojishughulisha na shughuli yeyote kwa madai kuwa wanasubiri serikali
iwaboreshee mazingira hivyo kusababisha kundi hilo kuzidi kuwa masikini
Amesema imezoeleka kuwa mtu akishaajiriwa na kuanza kupata
mshahara hutegemea mshahara huo tu jambo ambalo ameliita ni hatari kwa kuwa
mtua anayetegemea mashahara na akijishughulisha na shughuli za ujasiriamali
itasaidia kuzidi kuinua kipato chake
Dkt. Steven amesema elimua ya ujasiriamali inazidi
kuwajenga watu na kuboresha kipato cha mtu hivyo kuwataka vijana na wananchi
kwa ujumla kuacha kusuasua kufanya shughuli za kiujasiriamali kwani wale
wanaosuasua maisha yatazidi kuwa magumu kwao
Katika hatua nyingine amewataka wajasiriamali kutunza
mitaji kwani wajasiriamali wengi wamekuwa na tabia ya kula mtaji jambo
linalochangia kuwarudisha nyuma
No comments:
Post a Comment