Tanzania,
Taifa Stars leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika michezo ya
kirafiki
baada ya kuifunga Zambia 1-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Stars ambayo Novemba 14, mwaka huu
iliifunga 1-0 Kenya, Uwanja wa CCM Kirumba, walikuwa mbele kwa bao 1-0
lililowekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa.
Ngassa,
anayecheza kwa mkopo Simba SC akitokea Azam FC, zote za Dar es Salaam,
alifunga
bao hilo dakika ya 45, akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa Simba SC,
Mwinyi
Kazimoto.
Stars
ilicheza vizuri na kwa umakini wa hali ya juu kipindi cha kwanza, na
kufanikiwa
kuwabana mabingwa hao wa Afrika wanaojiandaa kwenda kutetea taji lao
nchini
Afrika Kusini mapema mwakani.
Kipindi
cha pili, Zambia walianza kwa kurekebisha kikosi chao, kocha Mfaransa,
Herve
Renard akiwatoa Hichani Himonde, Moses Phiri, Sinkala na Isaac Chansa na
nafasi
zao kuchukuliwa na Stopila Sunzu, Mukuka Mulenga, Evans Kangwa na
Francis
Kasonde.
Pamoja na
mabadiliko hayo, Stars iliendelea kung’ara na katika dakika ya 57 Ngassa
alikaribia kufunga tena kama si shuti lake kufuatia pasi ‘tamu sana’ ya
Sure
Boy kutoka nje.
Lakini
kukosa kwa Ngassa bao hilo, kulitokan
ya England, ambaye alimbana
kiungo
huyo wa Simba kumynima mwanya wa kupiga vizuri na akafanikiwa kumfanya
apige
nje.
Zambia
walipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha bao dakika ya 76, baada ya shuti
la
Chasamba Lungu kugonga mwamba, wakati kipa Juma Kaseja akiwa
amekwishapotea
maboya.
Ngassa
alijibu shambulizi hilo dakika ya 77 baada ya shuti alilojaribu kupaa
juu ya
lango, huku Felix Katongo akipewa kadi ya njano, baada ya kumuangusha
Amri
Kiemba aliyekuwa anamfunga tela.
Juma Kaseja
alifanya kazi ya ziada dakika ya 86, baada ya kuokoa shuti la karibu la
Chris
Katongo na katika dakika ya 87, Stars ilipata pigo baada ya beki Kevin
Yondan
kuumia na nafasi yake kuchukuliwa beki mwenzake wa Yanga, Nadir Haroub
Ally
‘Cannavaro’ dakika ya 88.
Taifa Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni,
Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan/Nadir Haroub dk 87, Frank
Domayo,
Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa/Amir Maftah
dk83 na
Khamis Mcha ‘Vialli’/Simon Msuva dk59.
No comments:
Post a Comment