JINA
la Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe limeendelea kutumiwa
vibaya na matapeli wa Mkoa wa Njombe ambao tayari wamewaibia watu
mamilioni ya shilingi, gazeti hili limebaini.
Imedaiwa kuwa matapeli
hao wamekuwa wakitumia jina la mbunge huyo kwa kupigia watu simu na
kuomba kutumiwa fedha kwa ajili ya jambo fulani au kukopa wakati siyo
kweli.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa tayari watu zaidi
ya wanane ambao hawakutaka majina yao kuandikwa gazetini, walipigiwa
simu na Filikunjombe feki kuombwa wamuazime kiasi fulani cha fedha au
kuchangia miradi ya kijamii nao kufanya hivyo wakiamini kuwa ni mbunge
wao.
Aidha, imegundulika kuwa mmoja wa matapeli hao amejisajili kwa jina la mbunge huyo na kuvuna fedha haramu.
Kiongozi
mmoja wa Kituo cha Radio Njombe alinusurika kutapeliwa baada ya
kumshitukia Filikunjombe feki, hivyo kukwepa kunasa katika mtego huo.
Kwa
upande wake, Mbunge Filikunjombe amesema: “Sina kawaida ya kumtumia mtu
au kuazima fedha kwa njia ya simu. Nawaomba wananchi wawe makini na
matapeli wanaotumia jina langu kutapeli.”
No comments:
Post a Comment