Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili nchini Tanzania na Afrika Rose Muhando anatarajiwa kuwapagawisha wakazi wa mkoa wa Iringa katika tamasha kubwa lililopewa jina la mlipuko wa lulu za injili likakalofanyika siku ya jumanne ijayo katika skikukuu ya ya Krismas kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Mratibu mkuu wa tamasha hilo Victor Chakudika ambae ni meneja wa kituo cha |radio Nuru Fm Iringa amesema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya tamasha hilo yamekamilika na kuwa zaidi ya wasanii sita kutoka nje ya mkoa wa Iringa na ndani ya mkoa wa Iringa watashiriki kutoa burudani katika tamasha hilo.
Chakudika alisema kuwa tamasha hilo ni maalum kwa wakazi wa mkoa wa Iringa katika kusherekea sikukuu ya Krismas na hivyo kuwataka wapenda burudani wote mkoani Iringa badala ya kwenda katika kumbi za miziki ya kidunia kwa siku hiyo kuweza kuungana na wakristo kote duniani katika kusherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo .
Hata hivyo alisema kiingilio ambacho kimewekwa kwa ajili ya tamasha hilo ni kidogo zaidi kwa ajili ya kuwawezesha watu wote kuweza kukusanyika pamoja na kupokea baraka za Mungu kupitia mwimbaji huyo Rose Muhando na wengine wengi ambao wataongozana na mwimbaji huyo.
No comments:
Post a Comment