Boniface Wambura, Ofisa Habari TFF |
Na Princess Asia
SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa
timu ya Coastal Union, Mussa Rico kilichotokea jana (Desemba 22 mwaka huu) jijini Tanga.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba, msiba huo ni
mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti akiwa mchezaji
Rico, na baadaye kocha alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na
kufundisha ikiwemo Coastal Union, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Amesema TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Rico, Chama cha Soka Tanga (TRFA) na klabu
ya Coastal Union na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki
kigumu cha msiba huo mzito.
Amesema mazishi
yanatarajiwa kufanyika leo (Desemba 23 mwaka huu) mkoani Tanga. Mungu aiweke
roho ya marehemu Rico mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment