Jeshi la polisi wilayani Makete linamshikilia mwanamke mmoja
mkazi wa Malembuli wilayani hapa kwa kosa la la kumzika mwanae wa kumzaa
mwenyewe na kutorokakea jijini Mbeya .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa polisi wilaya
Makete Peter Kaiza amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Bi Fatuma sanga mkazi wa
kijiji cha Malembuli mnamo tarehe 14
desemba mwaka huu Bi Sanga alimzika
mototo wake wakumzaa mwenyewe mwenye
umri wa mwezi mmoja.
Bwana Kaiza amesema Bi Sanga baada ya kutenda tukio hilo alitolokea jijini
Mbeya na polisi baada ya kupata tarifa
kutoka kwa raia wema walilazimika kumfuata na kufanikiwa kumkamata Bi
sanga ambaye atapelekwa mahakamani baada ya
uchunguzi kukumilika
Aidha inadaiwa kuwa Bi sanga alimzika mototo huyo nje kidogo
ya eneo analo ishi ambapo alidaiwa kuwa alimzika mototo huyo baada ya kufariki
dunia
Hata hivyo jeshi la
polisi likuwa likimshikilia Bi sanga pamoja na mmewe ambaye kwasasa ameachiliwa
baada ya maelezo ya Bi sanga kuwa mmewe hahusiki chochote na wala hakujua
chochote kuhusu tukio hilo
Bi sanga anatarajiwa
kufikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete
baada ya uchunguzi wa awali kukamilika
Hilo
ni tukio la pili kutokea katika kata hiyo baada ya tukio lingine lilitokea
mwaka 2009katika kijiji cha Makangalawe ambapo mwanamke mmoja alimtupa mototo
wa siku tatu katika mto masalala
No comments:
Post a Comment