DAKTARI wa kitengo cha upasuaji
katika Hospitali ya Rufaa Mbeya,Paul Kisabi (32), amefikishwa katika Mahakama
ya Mkoa wa Mbeya, akikabiliwa na mashitaka mawili ya kushawishi na kupokea
rushwa ya shilingi 100,000 kutoka kwa mgonjwa aliyefikishwa Hospitalini hapo
baada ya kupata ajali.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego. Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani majira ya saa 3:45 na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali kwa wananchi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Taasisi ya kuzui na Kuipambana na rushwa nchini takukuru, kumtia mbaroni daktari huyo juzi kwa tuhuma za kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha baada ya kumuwekea mtego. Daktari huyo Kisabi amepandishwa kizimbani majira ya saa 3:45 na kusomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mbeya, Fransis Kishenyi, aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo ambayo imeibua hisia kali kwa wananchi.
Katika kesi hiyo namba 237 ya mwaka
2012, upande wa mashitaka uliongozwa na waendesha mashita wawili wa Taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU), Joseph Mulebya na Nimrod
Mafwele.
Waendesha
mashitaka hao walidai kuwa Disemba 19 majira ya asubuhi akiwa katika sehemu
yake ya kazi katika kitengo cha upasuaji, mshitakiwa alitenda kosa la kwanza la
kushawishi rushwa ya shilingi 200,000 kutoka kwa mgonjwa Meshack Brown,
aliyefika hapo kwa lengo la kupatiwa matibabu.
Walisema katika kosa la pili, siku
hiyo majira ya saa nane mchana akiwa katika baa moja iliyojulikana kwa jina la
Victoria iliyopo Jijini hapa, mshitakiwa alitenda kosa lingine la kupokea hongo
ya shilingi 100,000, huku akijua kuwa vitendo vyote hivyo ni kinyume na sheria.
Walisema kuwa kwa mujibu wa sheria
za taasisi hiyo, makosa yote yaliyotendwa na mshitakiwa yanaangukia kwenye
kifungu cha 15 ibara ya 1 (a) cha sheria ya kuzuia rushwa namba 11 ya mwaka
2007.
Kabla kupangwa tarehe ya kutajwa
tena kesi hiyo, Wakili wa mshtakiwa huyo, Ladislaus Rwekaza,aliiomba mahakama
impe dhamana mteja wake akidai kuwa makosa yanayomkabili yanadhaminika.
Hakimu Kishenyi alikubaliana na
maombi ya Wakili Rwekaza kuwa mashtaka yote yanayomkabili mshtakiwa
yanadhaminika na kusema dhamana yake iko wazi.
Alimtaka mshtakiwa huyo kutimiza
masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini mali yenye thamani ya
Sh,500,000, na kwamba awe na utambulisho wa barua kutoka kwa kiongozi wa
serikali ya mtaa .
Hata hivyo mahakama ililazimika
kuahirishwa kwa muda wa dakika 20 ili kutoa nafasi kwa mdhamini wa mshitakiwa
kuleta barua hiyo baada ya kudai kuwa alikuwa ameisahau kwenye gari lililokuwa
nje ya jingo la mahakama.
Baada
ya kupokea ombi hilo hakimu Kishenyi aliwahoji waendesha mashitaka kama
wameridhika na hoja, ambao kwa pamoja walikubali kwa maelezo kuwa dhamana ni
haki ya kisheria kwa mshitakiwa hivyo hawakuwa na pingamizi.
No comments:
Post a Comment