SAKATA
la mnyama aina ya fisi kushambulia na kujeruhi mtoto mdogo katika
kijiji cha Kasahunga, wilayani Bunda, mkoani Mara, limechukua sura mpya
baada ya wananchi wenye hasira kuziteketeza kwa moto nyumba za mwananchi
mmoja wakimtuhumu kwamba ndiye anayemiliki fisi huyo kichawi.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji cha Kasahunga, Chriphord James Nyamega,
tukio hilo lilitokea usiku wa kuamka jana kijijini hapo.
Imeelezwa
kuwa hatua hiyo ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na vijiji jirani
kujichukulia sheria mkononi,imetokana na baada ya fisi waliyekuwa
wanamfukuza kupotea katika mazingira ya kutatanisha katika eneo la mji
huo.
Nyamega
alisema kuwa, siku tatu kabla ya tukio hilo majira ya jioni mnyama huyo
alimshambulia mtoto mdogo mwenye umri wa miaka saba na kumjeruhi vibaya
sehemu mbalimbali za mwili yake, wakati akitoka kutafuta kuni na
wenzake wawili.
Alisema
kufuatia tukio hilo, wananchi walilihusisha na imani za kishirikina, na
kuamua kufanya mkutano wa vitongoji vitatu vya Chang’ombe, Pida na
Songambele kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuwinda fisi hao ambao
inadaiwa kwa sasa ni kero kubwa kijijini hapo.
Alibainisha kuwa siku hiyo wananchi walianza msako wa kutafuta wanyama hao lakini hawakufanikiwa kuwapata.
Alibainisha kuwa siku hiyo wananchi walianza msako wa kutafuta wanyama hao lakini hawakufanikiwa kuwapata.
Alisema
kuwa kesho yake ulifanyika mkutano wa kijiji kizima ukishirikisha Ofisa
Mtendaji wa kata ambaye pia ni Kaimu Ofisa Tarafa ya Kenkombyo, Abiud
Jandwa pamoja na diwani wa kata hiyo, Sospeter Masambu, kwa ajili ya
kuzungumzia tukio hilo.
Katika mkutano huo, lilipitishwa azimio kuwa Jumanne ijayo zipigwe kura za siri kuwabaini watu wanaomiliki wanyama hao.
Imeelezwa
kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo, jioni fisi mmoja alionekana
katika eneo la kati la Kasahunga, jirani na ulikofanyika mkutano huo,
ambapo wananchi walimfukuza hadi kitongoji cha Songambele ambako alitaka
kukamata mtoto mmoja.
Wananchi
walipiga yowe na kumfukuza fisi huyo hadi kitongoji cha Kisiwani,
ambako inadaiwa kuwa alikamata mbwa kwenye mji wa mwananchi mmoja na
kutokomea naye kusikojulikana.
Fisi
huyo alionekana tena Saa 2:00 usiku, ambapo wananchi walimfukuza na
baada ya kufika katika eneo la nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, ghafla
alipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Kutokana
na hali hiyo wananchi wenye hasira walivamia nyumbani hapo na kuanza
kubomoa nyumba, zizi la mifugo, mabanda ya kuku na bata na kisha
kuziteketeza kwa moto nyumba mbili za mwananchi huyo.
Wananchi
hao pia inadaiwa walichukua ng’ombe mmoja na kwenda kumchinjia ziwani
na kugawana nyama, huku baadhi yao wakipora mifugo wakiwamo mbuzi, kuku
na bata.
Wakati hayo yakifanyika inadaiwa kuwa mwenye mji pamoja na familia yake, walishatoroka wakiogopa kushambuliwa na wananchi hao waliokuwa na silaha za jadi, ambapo hadi jana asubuhi familia hiyo ilikuwa haijulikani ilipo.
Wakati hayo yakifanyika inadaiwa kuwa mwenye mji pamoja na familia yake, walishatoroka wakiogopa kushambuliwa na wananchi hao waliokuwa na silaha za jadi, ambapo hadi jana asubuhi familia hiyo ilikuwa haijulikani ilipo.
Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment