MCHUGAJI wa kanisa
la aliyejulikana kwa jina ka Mchungaji Msyaliha wa usharika wa Mbalizi
wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya, alionja joto la jiwe makaburini
baada ya kupewa msokoto wa Bangi na vijana ambao walikuwa wakimzika
mwenzao.
Tukio hilo
lilitokea juzi eneo hilo la Mbalizi katika msiba wa kijana Denis Sanga
ambaye alifariki dunia kwa kile kinachoodaiwa kuwa ni ajari
iliyosababisha mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
Vijana hao baada ya
kumalizi kuchimba kaburi hilo walilazimisha kufunuliwa jeneza la
marehemu huyo na kuweka misokoto ya bangi huku wengine wakivuta
hadharani huku wakihamasishana mchungaji huyo apewa bangi.
Vijana hao
walisikika wakiimba '''Mpe bomba mpe bomba mchungaji hana hasira'' na
baadaye ukaletwa msokoto mkubwa wa bangi ili mchungaji huyo akabidhiwe
jambo ambalo lilimtia hofu mchungaji huyo kisha kuanza kukimbia na
kushindwa kutoa neno la Mungu.
CHANZO;http://kalulunga.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment