Ajali imetokea jioni wakati ndege hiyo ikielekea hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi ambapo meneja wa uwanja wa ndege wa Mpanda Mahamud Muhamed kasema ajali ilitokea jana december 16 2012 saa kumi na dakika 55 jioni.
Ni ndege ya abiria mali ya hifadhi ya taifa ya TANAPA na una uwezo wa kuchukua abiria wanne na imeanguka umbali wa kilometa moja na nusu kutoka uwanja wa ndege.
Rubani wa ndege hiyo alipata msaada kutoka kwa wananchi waliokuwa shamani mwao ambapo mmoja wao alisema wakati akiwa anafanya shughuli zake za kilimo ghafla aliona ndege angani ikizimika injini na muda mfupi baadae ikaanguka jirani na mti wa mwembe, kazi ya uokoaji ilichukua muda kidogo kutokana na nyuki.
No comments:
Post a Comment