Monday, December 10, 2012

ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUIBA MTOTO


MKAZI wa kijiji cha Mitundu, tarafa ya Itigi, wilayani Manyoni, Anna Wilsoni Mika Msinjili (31) amenusurika kuuawa na wananchi baada ya kutuhumiwa kuiba mtoto mchanga mwenye umri wa miezi saba.

Habari zilizopatikana kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji hicho, Festo Mlowezi, na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi wilayani Manyoni, zinaeleza tukio hilo lilitokea Desemba mosi mwaka huu, majira ya saa 3 asubuhi katika kituo kidogo cha polisi Mitundu.

Mwenyekiti huyo alisema chanzo cha mwanamke huyo kuiba mtoto ni kutofanikiwa kupata mtoto hata mmoja katika kipindi chote cha uhai wake na wala si kwa imani za kishirikina.

Alisema kabla ya tukio hilo, mama mzazi wa mtoto aliyeibwa, Mariamu Shaban (34) mkazi wa kijiji cha Mitundu alikuwa akifanya biashara zake mnadani; alimtuma binti yake mwingine, Joyce Masila anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 6 au 7 kwenda nyumbani kuleta nguo za kumbadilishia mtoto huyo.

“Wakati Joyce akiwa amembeba mtoto huyo, Asha Alfan alianza kulia na ndipo alipokutana na Anna ambaye alimwomba ambebe ili amsaidie kumbembeleza na kumtaka kwenda kufuata nguo alizotumwa nyumbani,” alisema mwenyekiti.

Alieleza kuwa baada ya Joyce kurudi hakumkuta mwanamke huyo na ndipo alipokwenda kutoa taarifa kwa mama yake.

“Mama huyo alipokwenda kutoa taarifa kituo cha polisi alikuta taarifa kuwa mtoto huyo alikuwa katika kitongoji cha Madole Tisa ndipo walipokwenda na kumkuta mtoto nyumbani kwa mtuhumiwa,” alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo alipofikishwa kituo cha polisi alikana kuiba mtoto huyo na kudai alikabidhiwa na mwanamke mmoja ambaye alitoweka, hali iliyoamsha hasira kwa wananchi waliokuwapo eneo hilo

No comments:

Post a Comment