Mh.Raisi Kikwete akiwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka
Ray C leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati mwanamuziki huyo alipoenda
kumtembelea Raisi na kumpa shukrani kwa kumsaidia kwenye matibabu ya juu ya
ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Aidha Ray C alimueleza Raisi kwamba afya yake
imeimarika na kwamba muda mfupi ujao atarudi kuendelea na kazi yake ya muziki.
Kwa upande wa mama yake Ray C amemshukuru Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanae
kwa kugharamia matibabu yote ya mwanae.
No comments:
Post a Comment