Kim Poulsen kushoto akiwa kocha wa vijana, Mdenmark mwenzake, Jacob Michelsen |
KOCHA Mkuu wa timu ya
soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
Mdenmark Kim Paulsen amemuorodhesha kipa Juma Kaseja katika kikosi cha
wachezaji
22 watakaounda kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kitakachomenyana na
Kenya, Harambee
Stars katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya FIFA (Shirikisho
la Soka
la Kimataifa) Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wiki ijayo.
Mbali na Kaseja wa Simba,
Kim aliyepandishwa kutoka timu ya
vijana mwaka huu akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen
amemuita
pia kipa Deogratius Mushi wa Azam FC.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari mjini Mwanza leo, Paulsen
aliwataja wachezaji wengine ni mabeki Kevin Yondan wa Yanga, Aggrey
Morris,
Erasto Nyoni wa Azam FC, Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Nassoro Masoud
‘Cholo’, Shomari Kapombe
na Amir Maftah wa Simba, wakati viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa
Azam FC,
Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa
wa
Simba, Athuman Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo wa Yanga na Shaaban Nditi wa
Mtibwa
Sugar.
Washambuliaji walioitwa
na Paulsen ni John Bocco ‘Adebayor’ wa
Azam FC, Simon Msuva wa Yanga, Christopher Edward wa Simba, Mbwana
Samatta na
Thomas Ulimwengu wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo
(DRC).
Tofauti na ilivyotarajiwa na wengi, Poulsen
hajamuita mshambuliaji Jerry Tegete wa Yanga, ambaye ameonekana kufufua
makali yake siku za karibuni.
Hata hivyo, Poulsen hakuchukua wachezaji wa Zanzibar
kwa
sababu nao watakwenda kujiunga na timu ya Zanzibar, inayojiandaa na
michuano ya
Kombe la CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa mwezi huu mjini Kampala,
Uganda. Alisema
hicho ndio kikosi anachotarajia kukutumia katika Challenge. Kambi ya
timu hiyo
itakuwa mjini Mwanza, kwa kuwa ni jirani na Uganda.
No comments:
Post a Comment