Kaseja kulia akizungumza na kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen hivi karibuni |
NAHODHA wa
Simba, Juma Kaseja amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia yeye na klabu
hiyo
basi.
rizikimgaya amefika kwenye mazoezi ya Simba
jioni ya leo Uwanja wa Kinesi, Urafiki, Dar es Salaam na kukuta
wachezaji wote
wakiendelea na mazoezi kujiandaa na mechi ya Toto African mwishoni mwa
wiki,
kasoro Kaseja na Amir Maftah.
Alipoulizwa
Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kwamba Maftah ana ruhusa
maalum
kwa sababu ameoa hivi karibuni, lakini Kaseja hawana taarifa zake, ila;
“Nadhani hatakuwa vizuri kisaikolojia baada ya kufanyiwa fujo
Jumamosi,”alisema
Kamwaga.
Lakini rizikimgaya ilipozungumza na wachezaji wenzake, walisema Nahodha wao
amewaaga kwamba yeye na Simba basi, kwani ameumia sana kwa jinsi
alivyodhalilishwa na mashabiki Jumamosi Morogoro.
“Juma hapa
ndio basi kaka, Kasema yeye na Simba basi, amesononeshwa mno na jinsi
alivyodhalilishwa baada ya mechi ya Morogoro,”alisema mchezaji mmoja wa
Simba
baada ya mazoezi Kinesi leo.
Kaseja alitukanwa
na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba baada ya mechi dhidi ya Mtibwa
Sugar
kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya
kizembe.
Lakini tayari
uongozi wa Simba umelaani vikali vurugu na vitisho alivyotolewa kipa wao
huyo namba
moja, na kusema wanafikiria kuwachukulia
hatua kali watu waliomfanyia hivyo Nahodha wao huyo.
Juhudi za kumpata
Kaseja mwenyewe kuzungumzia suala hilo, hazikuweza kufanikiwa kwani simu
yake
ilikuwa haipatikani.
No comments:
Post a Comment