Kanisa katoriki jimbo la Njombe limechangia zaidi ya
shilingi milion kumi na sita kuajili
ujenzi wa nyumba ya mwalimu
katika shule ya msingi Makangalawe wilayani Makete.
Akitoa taarifa
mbele ya wandishi wa habari mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Patrick Malumba
asema ujenzi wa nyumba hiyo utaghalimu zaidi ya shilingi milioni ishirini huku
wananchi wakichangia shilingi milioni nne na kanisa katoriki jimbo la Njombe
likichangia shilingi milioni kumi na sita.
Bwana malumba
amesema kuwa jengo hilo lilianza kujengwa September mwaka huu linatajia kukamilika ifikapo
desember 30 mwaka huu na kuanza kutumika mapema januari mwakani kwani shule
hiyo inakabiliwa na uhaba wa nyumba za walimu kukamilika kwa
jengo hilo kutasaidia kuongeza ufanisi kwa walimu na kuongezeka kwa ufaulu kwa
wanafunzi katika mitiani ya kitaifa alisema Malumba.
Mwisho bwana Malumba
aliwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kusaidia ujenzi huo pindi nguvu
zao zinapohitajika kwani mpaka sasa wapo
hatua za mwisho za bimu na muda mfupi wataanza uezekaji wa jengo hilo.
No comments:
Post a Comment