Urusi leo imeishutumu Marekani kwa kuratibu usambazaji wa silaha kwa waasi
wa Syria,
licha ya hakikisho la wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani kuwa haitoi msaada
wowote wa silaha.
Taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya
kigeni ya Urusi imesema Marekani inafahamu kuhusu usambazaji wa silaha
mbalimbali kwa makundi haramu yenye silaha nchini Syria.
Wakati huo huo, kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei
ameilaumu Marekani na Israel
kwa uasi unaoendelea kwa mwezi wa 19 sasa nchini Syria. Khamenei pia amezionya nchi
za Magharibi dhidi ya kuingilia mgogoro huo.
Katika hotuba yake kwa Waislamu
wanaoshiriki katika ibada ya Hijja mjini Makka, alisema vita vya wenyewe kwa
wenyewe vinavyowahusisha vijana wa Kiislamu kuuwana, ni uhalifu ulioanzishwa na
Marekani na utawala wa Israel, kuiadhibu Syria kwa kukataa uvamizi wa Israel na
kuyaunga mkono makundi ya Kipalestina na Lebanon yanayopinga Israel.
No comments:
Post a Comment