Uganda inatishia kujiondoa katika mazungumzo ya kuleta amani
katika nchi kadhaa barani Afrika.
Tisho hilo
linafuatIa ripoti ya Umoja wa mataifa iliyokashifu Uganda
kwa madai ya kuunga mkono makundi ya waasi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Waziri wa serikali , Asuman Kiyingi, alisema
kuwa dhana kuwa Uganda
inaunga mkono waasi wa M23 katika DRC wakati ikiwa mpatanishi mkuu katika
mazungumzo ya amani ni njama ya kuidhalilisha na kuiharibia sifa nchi hiyo.
Aliongeza kuwa , ikiwa madai hayo hayataondolewa
dhidi yake pamoja na juhudi za nchi hiyo kukosa kutambulika, serikali itaondoa
wapatanishi wake kwenye mazungumzo ya amani.
Amesema pia vikosi vya nchi hiyo vilivyo
nchini Somalia
na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, pia vitaondolewa.
Vikosi hivyo vinaungwa mkono na Umoja wa
Mataifa hatika harakati zao dhidi ya waasi na wanamgambo.
No comments:
Post a Comment