Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakao shawishi wananchi kwa lolote juu ya katiba.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akitoa taarifa ya ratiba ya tume ya katiba katika wilaya yake leo.
Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba Mpya Nchini Inatarajiwa Kuanza Ratiba yake ya Kukusanya Maoni Kuelekea Mchakato wa Katiba Mpya Wilayani Njombe Kuanzia Tarehe 27 Mwezi Octoba Mwaka Huu.
Akitoa Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusiana na Ratiba ya Tume Hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Dumba Amesema Tume Hiyo Itaanza Mikutano Katika Halmashauri ya Mji Njombe Kwa muda wa Siku Tano Kuanzia Tarehe 27 Hadi Tarehe 31 Octoba Mwaka Huu na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kuanzia Tarehe 1 Hadi Tarehe 5 Mwezi Novemba Mwaka Huu.
Akisoma Ratiba ya Tume Hiyo Bi .Dumb Amesema Tume Hiyo Itafanya Mikutano Miwili Kwa Siku Kwa Muda Wa Siku tano katika Halmashauri ya Mji Njombe na siku sita kwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Kutokana na Mazingira ya Kijiografia ya Wilaya Njombe.
Pia Bi.Dumba Ametoa Wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kwa uhuru bila kushawishiwa na watu wengine kwa siku zilizopangwa kwa kutumia utaratibu uliowekwa na Tume kutoa mapendekezo yao kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.
Kujitokeza kutoa maoni ni haki ya kila mtanzania ili kufanikisha mchakato wa uundwaji wa katiba mpya itakayowapa fursa wananchi wote kukipata kile wanancho kitaka bila shuruti na mtu yeyote.
No comments:
Post a Comment