Na Elisia Moshi, MAKETE
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Iwawa wilayani Makete
amelishukuru shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto ulimwenguni
(UNICEF) kwa kutoa msaada wa ujenzi wa vyoo shuleni hapo
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake mwalimu mkuu huyo
Bw. Fredy Chaula amesema kuwa vyoo hivyo havijakamilika rasmi ili kuanza
kutumika kutokana na ukosefu wa fedha za kuingizia maji katika vyoo hivyo
ambapo vyoo vinavyotumika sasa shuleni hapo sio imara
Amesema kuwa bado hajapewa na UNICEF gharama kamili za
fedha zitakazotumika kujengea vyoo hivyo na pindi atakapozipewa atazitoa kwa
uma
Amesongeza kuwa shule hiyo imekuwa na upungufu mkubwa wa
vitabu vya kufundishia na kujifunzia vya kiada na ziada na pia kuna upungufu wa
waalimu pamoja na ukosefu wa nyumba za kuishi waalimu
Hata hivyo ameiomba serikali kutimiza wajibu wake wa
kuongeza waalimu na vifaa vya kufundishia shuleni hapo pamoja na kujadili madai
ya waalimu pindi wanapotoa taarifa za madai hayo
Katika hatua nyingine shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi
394 ina waalimu 18 tu ambapo ameongeza kuwa waalimu hao hawatoshelezi kulingana
na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo shuleni hapo
No comments:
Post a Comment