Saturday, October 20, 2012

MRADI WA MAJI KIJIJI CHA NDULAMO WILAYANI MAKETE KUOKOA MAISHA YA WENGI

Na Furahisha Nundu, Makete
Zaidi ya shilingi milioni 20 zimetumika katika ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Ndulamo wilayani Makete mradi uliofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF
Akizungumza na Kitulo Fm afisa mtendaji wa kijiji cha Ndulamo Bw, Majuto Mbwilo amesema wananchi wa kijiji chake wamenufaika na mradi huo ulioanza kutekelezwa mwezi August mwaka huu na kumalizika mwezi huu
Amesema kuwa TASAF imechangia Tsh. Milioni 18, huku milioni mbili laki mbili sabini na sita elfu zimetolewa na kijiji hicho ambapo wameweza kukamilisha mradi huo kwa wakati muafaka
Mtendaji huyo ameishukuru TASAF pamoja na wananchi wa kijiji cha Ndulamo kwa kuonesha mshikamano tokea kuanza mpaka kukamilika kwa mradi huo kijijini hapo
Naye msimamizi wa mradi huo Martin Luvanda kutoka idara ya maji ya halmashauri ya wilaya ya Makete, amewataka wananchi wa kijiji hicho kutunza mradi huo pamoja na vyanzo vya maji vilivyopo kijijini hapo

No comments:

Post a Comment