Thursday, October 25, 2012

MAWAKILI SABA WAJITOA KESI YA VURUGU ZANZIBAR



Mawakili  wa Masheikh Saba wa Jumuiya ya Uamsho Salim Tawfik na Abdallah Juma   ,  wametangaza kujiondoa kwenye kesi hiyo  kutokana na madai ya usumbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuwahangaisha na kutowaleta mahakamani mara Kwerekwe mara Vuga.


 muda mfupi baada ya mawakili hao kuondoka na watuhumiwa ndio wakafikishwa mahakamani wakiwa wamenyolewa ndevu zote


JOPO la mawakili waliojitokeza kutetea viongozi wa uamsho Salim Taufiq na Abdallah Juma, wametangaza kujiondoa kwenye kesi hiyo wakati wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Mahakama ya Mwanakwerekwe kutokana na usumbufu wanaoupata wateja wao.


Muda mfupi baada ya mawakili hao kujitoa Masheikh hao waliwasili Mahakamani huku wakiwa wamenyolewa ndevu wote.


No comments:

Post a Comment