Wananchi wilayani Makete
wameshauriwa kutumia huduma za kibenki kutokana na elimu wanayoipata juu ya
huduma hizo
Akizungumza na wananchi
wa kijiji cha Iwawa Meneja wa benki ya NMB tawi la Makete Bw. Peter kinyosa
amesema kuwa benki hiyo inatoa huduma ya kuweka na kutoa fedha, mikopo pamoja
na kufungua akaunti kwa wateja wapya
Amesema matumizi ya
huduma za kibenki hayana usumbufu hivyo ni wakati muafaka kwa wananchi
kuhifadhi fedha zao benki kwani ni sehemu salama na yenye uhakika zaidi
Pia meneja huyo ametoa
wito kwa wateja wa benki yake kuhifadhi taarifa zao za siri za kibenki ili
kuepukana na wimbi la matapeli ambao wanaweza kuwaibia fedha zao
Naye afisa mikopo wa
NMB Makete Bw. Rodrick Mollel amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia mikopo
wanayoipata kufanyia shughuli za kimaendeleo ili kuinua kipato chao pamoja na
kunufaika na mikopo hiyo
Ameelezea changamoto
wanazokumbana nazo wakati wa kutoa mikopo kuwa ni usumbufu kutoka kwa wateja
wakati wa kurejesha fedha walizokopa pamoja na kutokuwa na viambatanisho muhimu
vinavyohitajika kabla ya kupewa mkopo
Na Elisia Moshi &
Hadija Sanga
No comments:
Post a Comment