Thursday, October 25, 2012

MASUPHA WAWEZESHA 112 MAKETE



 Jumla ya mbuzi 112 wamegawiwa kwa baadhi ya wanavikundi vya shirika la MASUPHAwilayani makete kwa lengo la kuboresha na kuinua uchumi wa vikundi  hivyo
  
      Akizungumza na rizikimgaya blogspot wakatiti wa ugawaji wa mbuzi hao mkurungezi wa shirika hilo Bi Aida Chengula amesema shirika hilo lilijadili kwa pamoja na wanavikundi hao ambapo wao wenyewe walipendekeza kuwa wanaitaji mbuzi wa kisasa  kwani wanauwezo kuwatunza na kuwahumia vizuri
  
         Bi chengula amesema baadhi ya vikundi hivyo vinavyo jumuisha walemavu na waishio wav vu ambao mara nyingi husaharika hivyo kwa kuwapatia mbuzi hao watainua uchumi wao
  
         Naye asisa ufuatiliaji tadhimini kutoka RFE Bwana Julius Mkandala ameongeza kuwa mbuzi hao itakuwa ni faraja kwa wanavikundi hao kwani watapata maziwa ya kuuza kunywa pia mbuzi kuuza kama njia mojawapo ya kujipatia kipato pamoja na mbolea kwajili ya bustani za mbogamboga
  
          Naye  mwanakikundi alijitambulisha kwa jina la Monica Mahenge kutoka Isapulano   ameeleza kufurahishwa na kufurahishwa na msaada huo kwani utamfanya ajikwamue na umasikini

Shirika la MASUPHA linalo jishighulisha na kuwahudumia wangonjwa wa UKIMWI na watu wenye ulemavu na limekuwa likisadia kwa kutoa misaada mbalimbali

No comments:

Post a Comment