
Wamiliki
wa maduka, bodaboda na grosali jijini Mbeya wamekumbwa na hofu baada ya
kuibuka kwa kundi la watu wanaodaiwa kuwa majambazi ambao wamekuwa
wakipora fedha na pikipiki katika maeneo tofauti tangu mwishoni mwa
Januari.
Mitaa
iliyoonja adha ya wavamizi hao ni ya Mafiati, Mwanjelwa, Mabatini,
Soweto na Mabanzini ambako vikundi hicho kilivunja maduka matano.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema wanashikilia watu watatu kuhusiana na matukio hayo.
Kamanda
Kidavashari alisema upelelezi wa awali unaonyesha kundi hilo limetokea
Tunduma mkoani Songwe na kwamba lilipokewa na wenyeji ambao huwaongoza
katika uporaji huo.
‘’Mpaka
sasa tunamsaka kijana anayeitwa Frank Senior au Frank Popo wa Mtaa wa
Iyela kwa madai ya kuhusika kusaidia uhalifu huo,’’ alisema.
Awali,
mwenyekiti wa wa Chama cha Waendesha Bodaboda Kanda ya Soweto, Joseph
Patrick alisema hivi karibuni kuna watu walifika eneo hilo saa 3:00
usiku wakawavamia madereva na kuwapora fedha, kisha wakavamia Mtaa wa
Block Q walikopora pikipiki mbili.
Aliwataja
walioporwa kuwa ni Saimon Nkwandi na Msafiri Jumanne. Patrick alisema
waporaji hao pia walimpiga risasi dereva mwingine aliyemtaja kwa jina la
Peter Hans baada ya kukataa kuwakabidhi pikipiki.
Mkazi
wa Mafiati, Betweli Mwakitabu alidai waporaji hao walivamia grosari
zaidi ya tano na kupora fedha kwa wamiliki na wateja. Tukio kama hilo
lilitokea pia Mtaa wa Mabanzini.
No comments:
Post a Comment