Serikali imetangaza kuwa kiwango cha
chini cha taaluma anayopaswa kuwa nayo
mwandishi wa habri kuwa ni ‘Diploma ya
Uandishi wa Habari’ kwa mujibu wa kanuni
za sheria mpya ya hunda za habari
zilizokamilika utungaji wake hivi karibuni.
Akizungumza na wana habari leo mjini
Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo , Nape Nnauye
amesema kuwa kanuni zimeshaundwa na
zimechapishwa kwenye gazeti la serikali
tangu Februari 3 mwaka huu baada ya
kupokea maoni ya wadau mbalimbali.
“Tumesoma, tumechambua maoni ya wengi,
wapo waliotaka iwe cheti, wengine diploma,
wengine digrii, wapo waliotaka PhD na wapo
waliotaka iwe mtu yeyote nayejua tu kusoma
na kuandika. Serikali imesimama katikati ya
maoni hayo. Sifa ya chini kabisa kwa kuanzia
itakuwa ni diploma ya uandishi wa habari”
Amesema Nape
Waziri Nape amesema pia kuwa sheria hiyo
imeshaanza kutumika tangu Desemba 31
mwaka 2016, ambapo yeye kama Waziri
mwenye dhamana alishatoa tangazo katika
gazeti la serikali.
Aidha kuhusu wasio na sifa hiyo, Waziri
Nape amesema kuwa serikali imetoa
kipindi cha mpito cha miaka mitano ili
waandishi wasiokuwa na sifa hiyo, waliopo
sasa na watakaoingia kwenye taaluma
hiyo, wakasome ili wawe wamepata sifa
hiyo.
Amesema katika utekelezaji wa sheria
hiyo, kuna taasisi ambazo tayari zipo,
zitaongezewa majukumu au kazi zake
kuhuishwa, pia kuna vyombo vipya
vitaanzishwa na kuna taratibu mpya za
kiutendaji zitaandaliwa.
Kuhusu manufaa ya sheria hiyo, Nape
amesema kuanza kutumika kwa sheria hiyo
ni jambo muhimu kwa tasnia hiyo kwa
kuwa ni ruhusa ya kuanza kwa mchakato
wa kuifanya taaluma ya habari kuwa
taaluma kamili yenye sifa mahsusi na
maadili yaliyokamilika pamoja na kuwa na
vyombo vya kusaidia utekelezaji wake.
Sheria hiyo ilisainiwa na Rais Magufuli
Novemba 16 mwaka 2016, na siku mbili
baadaye ilichapishwa kwenye gazeti la
serikali baada ya muswada wake
kupitishwa na Mkutano wa 5 wa bunge
mwezi Novemba 2016.
Sunday, February 5, 2017
Serikali yatangaza ‘Diploma’ ndiyo kigezo cha chini cha elimu kwa waandishi wa habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment