
Mahakama ya Rufaa nchini Marekani
imekataa kuirudisha tena marufuku iliyowekwa na Rais Donald Trump ya
wasafiri kutoka nchi saba za kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini
humo.
Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua
uamuzi uliotolewa na Jaji kutoka mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita
alizizuia sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.
Habari zinasema kwamba uamuzi huo kwa sasa utapelekwa katika Mahakama ya juu.
Na
muda mfupi tu baada ya Uamuzi huo wa mahakama kutangazwa, Rais Donald
Trum aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake
ataibuka mshindi.
''Ni uamuzi wa kisiasa na tutaenda kukutana mahakamani. Na natarajia
kufanya hivyo, Tuna hali ambayo usalama wa nchi yetu uko hatarini na ni
hali mbaya sana..'' Alisema Trump.
No comments:
Post a Comment