Friday, February 17, 2017

Maduka makubwa yafungwa kwa zaidi ya saa 4 kupisha zoezi la kuwaondoa machinga katikati ya jiji la Mwanza.

Baadhi ya maduka makubwa yaliyopo katikati ya jiji la Mwanza yamefungwa kwa zaidi ya saa 4, wakati askari polisi kwa kushirikiana na mgambo wa jiji hilo walipokuwa wakitekeleza agizo la kamati ya ulinzi na usalama wilayani Nyamagana la kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo waliovamia kwenye maeneo ya hifadhi za barabara kinyume cha sheria.

ITV imeshuhudia baadhi ya maduka katika mitaa mbalimbali yakiwa yamefungwa kwa hofu ya kuvamiwa na machinga, huku askari mgambo wa jiji la Mwanza pamoja na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia ( FFU ), waliokuwa na silaha za moto wakionekana kuimarisha ulinzi kila kona kwa kutumia defender licha ya baadhi ya wafanyabiashara waliozungumza na kituo hiki kuonesha kutoridhishwa kwao na utekelezaji wa zoezi hilo.

Kamera ya ITV imewanasa baadhi ya askari mgambo wakimshushia kipigo machinga mmoja aliyekuwa akitembeza nguo katika kituo cha daladala za Mwaloni.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wameunga mkono zoezi hilo la kuwaondoa machinga wanaodaiwa kuvamia kwenye maeneo yasiyo rasmi hasa kandokando ya barabara za Nyerere, Rwagasore, Kenyatta, Uhuru pamoja na eneo la msikiti wa Swaminalayani.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mary Tesha Onesmo anatoa maelekezo kuhusiana na wafanyabiashara hao na mahali wanapotakiwa kwenda kufanyia biashara zao.

Desemba 6 mwaka jana, rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli aliziagiza mamlaka mkoani Mwanza kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga waliokuwa tayari wameondolewa katikati ya jiji, hali iliyosababisha machinga hao kurejea na kufanya biashara kila mahali.

No comments:

Post a Comment