Wednesday, November 16, 2016

'Waliomtia' mwenzao kwenye jeneza hai washtakiwa

r Mlotshwa alikuwa akizungumza nje ya
mahakama ya mji wa kaskazini mashariki wa
Middelburg ambapo waliotaka kumshambulia
waliwasilishwa katika mahakama.
''Nilidhani wataniua'',alisema.
Kanda ya video ya dakika 20 iliorekodi kisa hicho
imekuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii
nchini Afrika Kusini.
Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani huko
Middelburg anasema kuwa ndani ya mahakama
hiyo ,washtakiwa hao ,Theo Martins Kackson na
Willem Oosthuizen,walisimama wakiwa
wameinamisha vichwa vyao chini huku waandishi
wa habari na raia wakichukua picha zao.
Wameshtakiwa kwa kumteka nyara na
kumshambulia kwa lengo kumjeruhi
vibaya.Hawajakubali ama kukana mashtaka hayo.
Wawili hao wanazuiliwa hadi tarehe 25 Januari
huku waendesha mashtaka wakisema kwamba
walihitaji muda zaidi kuchunguza ,ikiwemo
kuthibitisha video hiyo.
Mamake bw Mlotshwa alijawa na hasira na
kushindwa kujizuia wakati wa kusikizwa kwa
kwesi hiyo.Nje ya mahakama kulikuwa na kelele
za wafuasi wa vyama vikuu nchini humo huku
#RacismMustFall ikisambazwa katika mitandao
ya kijamii.

No comments:

Post a Comment